“Ni muda mrefu nimekuwa nikifuatilia mienendo ya mume wangu kutokana na tabia yake kubadilika sana siku za hivi karibuni, nikabaini kuwa kuna msichana anawasiliana naye kwa kutumiana meseji za mapenzi, sikuwa na haraka nikaamua kufanya uchunguzi wangu kimyakimya”
“Wiki iliyopita mume
wangu akiwa amekwenda kuoga akasahau kuzima simu yake,na siyo
kawaida yake kuacha simu yake bila kuizima,mara meseji
ikaingia,nikaangalia nikaona jina la mtumaji amesevu Lulu, moyo
ukalipuka”
Ndivyo alivyoanza kuongea mama mmoja wa makamo
anayefanyakazi katika ofisi moja nyeti katikati ya jiji la Dar
alipokuja kuongea na mwandishi wetu wiki iliyopita baada ya
ndoa yake kuingiliwa na mdudu mbaya….
Akiongea kwa masikitiko makubwa, mama huyo ambaye hakupenda
kutaja jina lake kutokana na unyeti wa kazi anayoifanya, alidai
kuwa msichana huyo anayetaka kuiharibu ndoa yake yenye miaka
25 jina lake ni Elizabeth Michael….
Mama huyo alidai kuwa jina hilo alilibaini baada ya
kukuta meseji za mapenzi kwenye simu ya mume wake na yeye
kuamua kuifuatilia namba hiyo kwa kufanya kama anataka kumtumia
pesa msichana huyo na kukugundua jina hilo….
Akiongea kwa upole, mama huyo alidai kuwa katika simu ya
mume wake, jina la mtumaji lilikuwa Lulu, lakini alipofanya
uchunguzi wake wa kujifanya kama anatuma pesa kwa namba ya
msichana huyo ndipo alipobaini kuwa mmiliki wa namba hiyo ni
Elizabeth Michael…
Mwandishi alimuuliza mama huyo kama anadhani kuwa msichana
huyo anayetaka kuiharibu ndoa yake ni muigizaji maarufu wa
filamu hapa nchini Elizabeth Michael “Lulu”, lakini alikataa
kuthibitisha hilo kwa madai kuwa tangu siku hiyo namba ya
binti huyo imekuwa haipatikani….
“Baada ya kugundua siku
ile , nilichukua simu yake na kutaka kuwasiliana naye ili
niweze kumuonya mwenyewe kimyakimya kwa wakati wangu, wala
sikuwa na lengo la kuja kwenye vyombi vya habari , lakini
sikuwahi kumpata hewani tena kila nilipojaribu kumpigia”Alisema na kuongeza:
“Huenda mume wangu
alishtikia kuwa nimeona ujumbe ule, kwa sababu mimi nilipoisoma
meseji ile sikuifuta, ili akiona meseji imesomwa aelewe
nimeshajua kila kitu, pengine ndiye aliyemwambia binti huyo
abadili namba yake”
Mwandishi alimuomba mama huyo ampatie namba ya huyo
msichana ili kuweza kujua kama ni Lulu muigizaji ama siyo (
mwandishi anazijua namba zote za Lulu ), lakini namba hiyo ni
tofauti na anazotumia Lulu Mwenyewe….
Mwandishi alipojaribu kama kumtumia pesa msichana huyo, jina
lililotokeza ni Elizabeth Michael, na alipojaribu kuipiga namba
hiyo ilikuwa haipatikani hewani….
Juhudi za kumsaka Lulu ili kuona kama anaitambua namba
hiyo hazikuzaa matunda kutokana na namba zake mbili
kutopatikana na nyingine ikiita bila kupokelewa….
Angalizo:
Baadhi ya wasichana wa mjini wamekuwa wakitumia majina ya
wasanii maarufu katika nyendo zao ili kuwatapeli watu. Miongoni
mwa njia wanazotumia ni pamoja na kujisajili kwenye mitandao
ya kijamii kwa majina ya watu maarufu ili kuwatapeli watu.
0 comments:
Post a Comment