Wednesday, June 11, 2014

 Kila mtu maarufu hapa Bongo anakitu cha kwanza ambacho ndio kilimtoa. Kwa Agness Gerald ilikuwa ni ile video ya nyimbo ya 'Masogange' aliyoimbwa na Msanii Belle 9 ambayo yeye alikuwa video queen. Tokea Video ya Masogange kubamba sana pande za Bo ngo ndipo Agness alipobatizwa jina la Masogange na kusifiwa kwa kuwa na mshape wa kufa mtu kwa upande wa video queens hapa Bongo. Hadi leo ukitaja video queen wenye shape ya ukweli basi wa kwanza kumtaja atakua ni Agness Masogange.

Agnes Masogange
Baada ya kushika chati kwa muda sasa, video queen mwingine kutoka Arusha , Hellen aliyeshirikishwa kwenye video ya wimbo wa Nikk Wa II 'Nje Ya Box' anaonekana kutaka kuchukua mikoba ya Masogange. Demu huyu ambaye kwa plan za mwanzo hakutakiwa kutokea kwenye video ya 'Nje Ya Box' kwakuwa kulikua na video queen mwingine aliyekimbia dakika za mwisho na yeye kuchukua mikoba hiyo anamvuto na umbile zuri na la kuvutia na niwazi aktokea kwenye video nyingine chache basi tutamsahau masogange.

0 comments:

Post a Comment

bb