Picha
chafu zinazodaiwa kuwa za star wa filamu nchini Shamsa Ford na mbunge
wa Chadema, Salvatory Machemli zimeanza kusambaa kwa kasi mitandaoni
tangu jana,. Picha hizo zinawaonyesha wawili hao wakiwa kitandani kwenye
mahaba mazito. Hata hivyo picha hizo zinatia shaka kuwa sio halisi ni
za kutengenezwa ingawa hatuna uhakika kwa asilimia zote kwasababu
msichana anayedaiwa kuwa Shamsa Ford ana umbo tofauti na la star huyo,
Shamsa ana umbo la kawaida ki-shape lakini msichana huyo anaonekana kuwa
na umbo namba nane.
Jana
baada ya kuona picha hizo ambazo zimeenezwa hasa kwenye pages za
kisiasa kwenye mitandao ya kijamii zikimuandama mbunge huyo wa
ChademaSwahiliworldplanet ilimtafuta Shamsa na kumueleza kila kitu na
kwa kujiamini Shamsa alisema sio zake hizo picha zimetengenezwa na pia
msichana anayeonekana kiumbo wako tofauti na hata sura na akasema
anajiheshimu sana na ana familia yake asingeweza kufanya jambo kama
hilo, alipoulizwa je anafahamiana na Mh. Salvatory Machemli pia alikana
kujuana nae achilia mbali kuwahi kukutana nae "zimedaiwa kuwa ni mimi
but sio mimi, naomba uangalie hizo picha vizuri au kama upo WhatsApp
nikutumie halafu uone je ni mimi? kabla sijakujibu" Shamsa alifunguka
Star
huyo anayefanya vizuri na filamu kibao aliendelea kwa kusema "si umbo
hata sura ni tofauti, sijawahi hata kumuona huyo mheshimiwa, nahisi ni
watu ambao wananichukia wanataka kunichafua, kiukweli nawaomba mashabiki
wangu kabla ya kuanza kunihukumu waziangalie kwanza hizo pictures
vizuri, mimi nina familia na najiheshimu"
Kwa
upande mwingine baadhi ya wachangiaji mitandaoni wamedai kuwa picture
hizo ni za kutengenezwa kwasababu Mh.Machemli ana kitambi lakini katika
picha hizo hazimuonyeshi akiwa na kitambi, wengine wamesema kuwa picha
hizo zimechukuliwa katika mtandao mmoja wa ngono na kufanyiwa photoshop
lengo lake likiwa ni la kumchafua kisiasa mbunge huyo ambaye anadaiwa
kukumba na misukosuko ya mara kwa mara. Hata hivyo ukweli wanaujua
wenyewe.
NB. Tumeshindwa kuziweka picha hizo zikiwaonyesha mwili mzima kutokana na sababu za kimaadili.
0 comments:
Post a Comment