Tuesday, June 10, 2014

MSANII mwenye sauti mwanana anayetesa kwenye Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’, amefunguka kuwa, ndoa yake na mpenzi wake Nagari Kombo ‘Kaka wa Bongo’ inanukia.

Linah alisema hayo wikiendi iliyopita aliponaswa akijiachia na Kaka wa Bongo katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar ambapo mpango mzima wa Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 – 2014 ulikuwa ukifanyika.
lina na bf 
Linah akipozi na mpenzi wake Nagari Kombo wakati wa utoaji tuzo za Kili.
linah 
Msanii mwenye sauti mwanana anayetesa kwenye Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’.

“Sina haja ya kuendelea kumficha mpenzi wangu, kwani kwa sasa anatambulika kwa kila mtu na hasa ndugu zangu wa karibu, kitu cha kusubiriwa kwa sasa ni tarehe ya ndoa yetu tu,” alisema Linah.
LINAHNANAGARI 
Lina akiwa na mpenzi wake.
Kaka wa Bongo alijizolea umaarufu siku za nyuma baada ya kuingia uwanjani na kumkumbatia mchezaji, Ricardo Kaka wa Timu ya Taifa ya Brazil iliyokuwa ikichuana na Taifa Stars katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

0 comments:

Post a Comment

bb