Tumezoea kuona wasanii wa Tanzania wakiomba kufanya collabo na
wasanii wakubwa wa kimataifa kwa lengo la kujitangaza kimataifa, lakini
Diamond Platnumz amefikia hadhi ya yeye kuombwa collabo na wasanii
wakubwa.
Kundi la Mafikizolo la Afrika Kusini limemuomba hit maker wa
‘Number 1′ Diamond Platnumz afanye nao collabo, na jana (June 9)
waliingia katika studio ya Oskido iliyoko Johannesburg kurekodi wimbo
huo.
“We doing a collaboration with Diamond,the song is sounding awesome yes” aliandika Theo Kgosinkwe wa Mafikizolo katika moja ya picha wakiwa studio na Diamond.
Collabo hiyo ya Mafikizolo na Diamond itampa nafasi nzuri zaidi
Platnumz sababu ya ukubwa walionao wanamuziki hao wa Afrika Kusini.
Mafikizolo ni washindi wa Tuzo mbili za MTV (MAMA) 2014 zilizofanyika Jumamosi iliyopita huko Durban, Afrika Kusini.
0 comments:
Post a Comment