Husna mwigizaji wa Filamu
MWIGIZAJI wa kike wa filamu Bongo Husna Chobis ‘Awena’ amesema kuwa
baada kurudi katika biashara zake nje ya nchi yupo tayari kuolewa lakini
kwa mtu mwenye fedha na si mbabaishaji ambaye hawezi hata kumiliki
Bajaji hamuitaji, lakini kwa wale ambao wanaona wanajiweza kuwa
wachapakazi na wanapata fedha ya kubadilisha mboga.
Husna katika pozi
Husna Chobis
“Kuzaliwa katika familia ya
kimaskini ni bahati mbaya, lakini kuchagua mume maskini ni uzembe na
haustaili msamaha, ukitembea unajifunza mambo ya mastaa wa Ulaya
wanavyoishi wanapotaka kuolewa wanatafuta wanaokwenda nao kimaslahi,
hata mimi nahitaji mtu wa kueleweka na kipato pia,”anasema
Husna.Mwigizaji huyo aliyejizolea umaarufu katika filamu za kiasili
hasa filamu ya Ndase, anasema moja ya matatizo ya ndoa za kitanzania au
kiafrika ni kukosa uchaguzi na kuingia katika uhusiano wa kupotezeana
muda kisha kutengana kutokana na kuwa uzembe wa kukosa maamuzi kutoka
kwa wanawake wengi.
0 comments:
Post a Comment