Mwanzilishi na mmiliki wa Facebook, Mark Zuckerberg ameitwa na
mahakama ya Iran kujibu tuhuma za uvunjifu wa haki za usiri/faragha na
kuingilia mambo binafsi.
Maafisa wa Iran wameliambia shirika la habari la ISNA kuwa Zuckerberg
anatakiwa kufika katika mahakama iliyopo jimbo la Fars ambapo kampuni
yake ya Facebook na mitandao inayoimiliki kama WhatsApp na Instagram
inatuhumiwa kuvunja sheria.
Mahakama hiyo inamtaka Zuckerberg au mwanasheria wake kufika katika
mahakamani na kwamba endapo hatahudhuria mitandao hiyo itafungiwa na
huenda akalipishwa faini.
Wito huo unakuja ikiwa ni wiki moja imepita tangu vijana sita wa Iran
kukamatwa baada ya kupost video inayowaonesha wakicheza wimbo wa
Pharrell Williams ‘Happy’ wakiwa juu ya paa la nyumba huko Tehran.
Imeripotiwa kuwa muongozaji wa video hiyo bado yuko rumande.
0 comments:
Post a Comment