Wednesday, June 11, 2014

Wote mpaka sasa tunafahamu toka siku nyingi kwamba Diamond Platnumz ni mwimbaji pekee kutoka Tanzania aliechaguliwa kuwania tuzo kwenye tuzo za MTV BASE ambazo zinatolewa leo June 7 2014 hapa Durban South Africa ila kuna mengine mapya yamejitokeza hatukuwa tunayafahamu.
1.Diamond alipokelewa kistaa na kama mastaa wengine wote walivyopokelewa ambapo meneja wake Bab Tale anasema ‘imefika sehemu unaona kabisa jamaa wanatukubali sasa hivi, Airport tumepokelewa na magari matatu… mi sijawahi kupokelewa na kuendeshwa na Mwanamke mzungu yani ila kiukweli Diamond amepokelewa kifahari kama wengine’
2.Babtale amethibitisha kwamba Diamond ndio atakua msanii wa kwanza kufungua show leo kweye utolewaji wa tuzo hizi ‘kitendo cha msanii kupewa nafasi ya kufungua, kwa sababu MTV ni kubwa…. kitendo hicho ni kikubwa kwa msanii pia‘
‘Wakati wa mazoezi tulikutana na  Mafikizolo wasanii kutoka Afrika Kusini ambao wamekuja wenyewe kuomba kolabo na Diamond, wao wenyewe wanasema bwana tunaomba kolabo na wewe…….. sisi tulitakiwa kurudi bongo Jumapili lakini wao ndio wamesema watalipia gharama za sisi kuendelea kukaa hapa na mabadiliko ya ticket yetu ili turudi Tanzania Jumanne’ – Bab Tale

‘Hatukua tunajua kwamba Diamond ndio atafungua show kwenye utolewaji wa tuzo hizi za MTV, jana wakati tukiwa kwenye mazoezi ndio tukaambiwa’
‘Muziki unahitaji elimu na kujitambua, hata Mafikizolo walivyokuja kwetu wanasema kabisa wanahitaji umoja wa Afrika wakati nyumbani bongo tu yenyewe kwa wenyewe hawazimiani, Mafikizolo walivyofanya mkutano na waandishi wa habari yani kwa jinsi walivyoelezea kuwa na ndoto ya kufanya kolabo na Diamond….. imeonyesha ni jinsi gani Diamond ana nguvu’ – Bab Tale
Msimamizi mwingine wa Diamond ni meneja Mkubwa Fela ambae amethibitisha kwamba kwenye safari yake ya kuja South Africa ameambatana na Watanzania wengine saba ila kilichomfurahisha zaidi ni kwamba amekuja kukuta washkaji zake zaidi ya 20 wanaoishi Durban wameshanunua ticket tayari kwa ajili ya kumshangilia Diamond’
Wakati wa chakula cha jioni, Ommy Dimpoz ambae nae yuko hapa Durban alitania baada ya kuisikia hiyo habari kwenye AMPLIFAYA na kusema ‘yani sipati picha Diamond akishinda ile tuzo, shangwe zitakazotoka kwa hawa wabongo ni kama goli la Taifa stars’
Watanzania waliofunga safari kutoka Tanzania mpaka Durban ni pamoja na Wema Sepetu, Aunt Ezekiel, Bab Tale, Salam ambae pia ni meneja wa Diamond, Mkubwa Fela, Watangazaji Sam Misago, B12, Adam Mchomvu, Millard Ayo, Shadee lakini pia Nancy Sumari na mpenzi wake Lucas, Ommy Dimpoz, Shetta na mpiga picha Michael Carter Mlingwa

0 comments:

Post a Comment

bb